Image
Image

Watu 6 wafariki baada ya jengo la ghorofa kuporomoka magharibi mwa India.


Watu 6 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine wengi kukwama baada ya jengo moja la ghorofa tatu kuporomoka katika mkoa wa Maharashtra ulioko magharibi mwa India.
Jengo hilo linaarifiwa kuporomoka siku ya Jumanne usiku kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha nchini India.
Hadi kufikia sasa miili ya watu 6 waliofariki imeweza kutolewa huku shughuli za kuwaokoa wengine wengi zikiendelea katika eneo la tukio.
Idadi ya vifo inahofiwa kuongezeka kwa kuwa bado kuna watu wengi zaidi waliokwamia kwenye mabaki ya jengo hilo.
Wakati huo huo, viongozi wa shirika la kukabiliana na maafa nchini India pia wamearifu kuokolewa kwa watu 10 waliofikishwa hospitalini kutokana na majeraha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, jengo hilo la ghorofa linalosemekana kujengwa mwaka 1972, lilifanyiwa ukaguzi na wataalamu wa ujenzi siku chache zilizopita na kuthibitishwa kutokuwa imara.
Baadaye ilani zilitolewa za kuamuru watu kuondoka kwenye jengo hilo ingawa wengi walipuuzia na kusita kuondoka.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment