NAHODHA wa timu ya Azam FC, Himid Mau amekiri kupata upinzani mkali
katika mechi yao ya kirafiki na ya kumalizia ratiba ya mazoezi visiwani
Zanzibar na JKU iliyochezwa juzi Amaan mjini hapa.
Mau alisema kuwa pamoja na timu yao kuibuka na ushindi, lakini
wamepata wakati mgumu kuivaa ngome ya wapinzani wao hao ambao
walijiandaa kwa kila idara. Mau aliyaeleza hayo juzi usiku mara baada ya
kumaliza mchezo wao wa kirafiki na timu hiyo ambapo waliweza kushinda
mabao 2-0.
Alisema kuwa timu ya JKU ni timu nzuri ambayo kama itaweza kupata
mechi zaidi za kirafiki za kimataifa wanaweza kufanya vizuri katika
michuano yao kimataifa watakayoshiriki.
“JKU ni timu nzuri ambayo ni mechi pekee ambayo tumeongeza kitu kati
ya mechi zetu tatu tulizocheza, na sisi tumeshinda kutokana na udhoefu
tu lakini JKU kiboko”, alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa mchezo wao ulikuwa mzuri kwa kila upande na
kuendelea kusifia kiwango kizuri kilichooneshwa na wapinzani wao hao
ambao waliwafunga kwa udhoefu. Katika mchezo huo Azam ambayo ilitarajiwa
kuondoka jana, mabao yake yalifungwa na John Boko dakika ya 65 na
Abubukar Sure Boy dakika ya 85.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment