Image
Image

Kanyaga-twende ya mama Samia yamalizika Singida na kuanza Dodoma.

Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais ka tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akitoka Singida mjini kwenda Dodoma, kupitia Ikungi na Manyoni kufanya mikutano ya kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi, Gishuli Charles, alipowasili eneo la Makyungu, kufanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida Kaskazini lililopo katika wilaya hiyo ya Ikungi. Kushoto ni Katibu wa CCM, Ikungi, Aluu Sagamba.
Wananchi wakimshangilia Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili eneo la Makyungu kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida Kaskazini, wilayani Ikungi.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Makyungu jimbo la Singida Kaskazini.
Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Kone akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi.
Kada wa CCM aliyeko katika kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM akionyesha furaha kutokana na mambo kwenda vizuri katika mkutano wa kampeni wa Makyungu,jimbo la Singida Kaskazini.
                            Eti, CCM haina vijana! kwani hawa ni Wazee?
Mzee Maarufu kwa jina la Mzee Jeuri aliyekuwa Kada wa Chadema, akizungumza baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo wa Makyungu.
Mzee jeuri akisalimiana na mgombea mwenza wa Urais Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kuichana Chadema jukwaani, akisema kuwa chama hicho kimeua upinzania nchini kwa kumkaribisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, Edward Lowassa ambaye sasa ndiye mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema.
                     Wananchi wakizidi kushamiri kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akiwa amewabeba watoto Hussein na Hassan waliokuwa kwenye mkutan wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia kwenye eneo la Makyungu, Ikungi.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Jonathan Njau akisalimia wananchi alipotambulishwa kwenye mkutano huo wa Makyungu.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Jonathan Njau akiomba kura kwa wananchi alipotambulishwa kwenye mkutano huo wa Makyungu.
Wananchi wakisikiliza Katibu Mkuu wa UWT, AminaMakilagi wakati akimkaribisha Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia kwenye mkutano huo wa makyungu.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akihutubia wananchi kwenye mkutano huo wa Makyungu, Ikungi mkoani Singida
Mwandishi wa habari nguri wa TBC, Emmanuel Amas akiwa kazini wakati msafara ukielekea Dodoma baada ya kumalizika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais Mama Samia.
Masafara wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukienda Manyoni kupiga mkutano mwingine wa kampeni
 Wananchi wakiwa kwenye mnara wa kumbukumbu, kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni, kumsubiri Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM Manyoni.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM Manyoni.
Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati, akimuombea kura Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli,katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akihutubia mkutnao wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM, Manyoni.
BAHI-DODOMA
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano wa kampeni, katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma.
Wananchi wakiwa katika shamrashamra kumpokea Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia alipowasili jimbo la Bahi kuhutubia mkutano wa kampeni.
Mama Samia akiagana na baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa wa Singida waliomsingiza hadi Bahi mkoani Dodoma.
Mgombea Mwenza wa Uras kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCm mkoa wa Singida waliomsindikiza hadi Bahi Dodoma. 
 Wananchi waliofurika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma.
Baadhi ya viongozi waliopo kwenye msafara wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni jimbo la Bahi mkoani Dodoma
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida, Diana Chilolo akimuombea kura Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Bahi mkoani Dodoma.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimnadi mgombea Ubunge, wa Bahi Omari Badwel, mkutano wa kampeni uliofanyika leo kaika jimbo la Bahi mkoani Dodoma leo. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment