Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini, mazungumzo kati ya
Kaseja na viongozi wa klabu hiyo yako katika hatua za mwisho na wakati
wowote anaweza kusaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Mbeya City wameamua kufanya
mazungumzo na Kaseja kutokana na kufahamu uzoefu wake kwenye ligi hiyo
ambayo msimu ujao inatarajiwa kushirikisha timu 16 kutoka mikoa
mbalimbali nchini.
Hata hivyo, maamuzi ya kumsajili nyota huyo, yanapingwa na baadhi
ya mashabiki wa Mbeya City ambao ni wapenzi na wanachama wa Yanga.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, aliliambia gazeti hili
jana saa 11:52 jioni kwamba bado hawajasaini mkataba lakini wako kwenye
mazungumzo na kipa huyo ambaye aliwahi pia kuzidakia Simba, Moro United
na timu ya Taifa (Taifa Stars).
Kaseja kwa sasa ni mchezaji huru lakini bado anakabiliwa na kesi ya
madai iliyofunguliwa na Yanga ambao wanadai nyota huyo alikatisha
mkataba huku pia kipa huyo akisema klabu hiyo ilivunja mkataba naye kwa
kushindwa kumlipa sehemu ya pili ya malipo yake ya usajili ya Sh.
milioni 20 kama walivyokubaliana kwenye mkataba.


0 comments:
Post a Comment