Recep Tayyip Erdogan katika hotuba yake aliotowa katika hafla ambayo mkuu wa majeshi Necdet Ozel alimuachia uongozi jenerali Hulusi Akar, alizumgumzia kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliotokea siku za nyuma.
Rais Erdogan alifahamisha kuwa magaidi wanaotaka kuyumbisha usalama na kuharibu umoja wa raia wa Uturuki wataendelea kupata majibu kama inavyostahili.
Erdogan alizidi kufahamisha kuwa magaidi wanaoendesha mashambulizi wataulizwa kwa kila kitendo wanachotenda dhidi ya raia.


0 comments:
Post a Comment