Image
Image

Mh.Lowassa asababisha SUNAMI kwenye uzinduzi wa kampeni Jangwani.


Mgombea  urais  wa  vyama  vinavyounda  katiba ya  wananchi  UKAWA  Mh.Edward  Lowasa  ameongoza  maelfu   ya  wananchi  kuzinduzi  rasmi   kampeni  za  vyama hivyo  katika  uwanja  wa  jangwani  huku  akiwataka  wataanzania  kuhakikisha  wanapokea  mabadiliko kwa  amani  kwani  kwa  sasa  haya kwepeki.

Akizungumza   na  maefu  ya  wananchi katika  uzinduzi  huo  Mh.Lowasa  ambaye  amesema akichaguliwa  kuwa  raisi  atahakikisha  sekta zote  ambazo  zimezorota  kutokana  na  kukosa  usimamizi  ikiwemo  Elimu ,Kilimo ,na sekta ya usafirishaji ukiwemo wa reli na  Anga.

Kwa upande  wake  mgombea  mwenza Mh.Duni Haji amesema  maelfu  ya  wananchi  na viongozi  wanaendelea  kuunga  mkono  mabadiliko  ni ishara  ya  kutosha  kuonyesha  kuwa  wamechoshwa  na  uonevu  na  mabavu  ya  serikali  ya CCM.

Ukafika  wakati   wa viongozi  mbalimbali wa UKAWA wakiongozwa  na Mwenyekiti wa CHADEMA  Mh.Fereeman Mbowe ambao  wamesema dalili ya kwanza ya kuonyesha kuwa  viongozi  wa  CCM  hawathamini  wananchi  ni kujifanya  maskini  huku  wakificha  utajiri   wao.

Baadhi  ya   mawaziri  waliokihama  chama  cha  mapinduzi  akiwemo  Mh.Fredrik  Sumaye  na  Laurence  Masha  ambao  pamoja  na  kumpongeza Mh.Lowasa  kwa kuongeza  mabadiliko  wamesema waliyatamani  siku  nyingi  lakini  alishindwa  kwa sababu  ya  mfumo  ulioandaliwa  kwa  makusudi  ya  kuwatia  hofu  na  kuwatisha  huku  wakielezea  baadhi ya maovu  yanayofanyika  chini  ya  serikali  ya  CCM.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment