Image
Image

News Alert:UKAWA sasa rasmi kuzindua kampeni zao jangwani Jumamosi.

Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni  yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene imesema kuwa hafla hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.
Viongozi hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment