Image
Image

Benki ya Dunia:Tanzania yaongoza duniani kutoa huduma za pesa kwa simu.



Tanzania ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, Benki ya Dunia imesema na kuongeza kuwa Tanzania ni moja ya masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu.
Benki hiyo ya Dunia pia imesema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani na kulingana na uwezo wake.
Benki hiyo pia imesema kuwa nchi jirani ya Kenya inaongoza kwa kutuma pesa kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani.
“Huuni mfano kutoka Afrika ambao unaweza kuigwa na nchi zote duniani,” amesema Profesa Kaushik Basu, Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB) wakati akiwasilisha kwa ufupi tu yaliyomo katika Ripoti ya Benki hiyo ya World Development Report ambayo itatolewa hivi karibuni.
Profesa Basu alikuwa anazungumza jana, Jumatatu, Septemba 28, 2015 kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliozungumzia Hali ya Enzi za Digitali (Digital Age) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni sehemu ya majadiliano kuhusu Malengo ya Maendeleo Mapya (SDG’s) ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) ambayo muda wake wa utekekezaji wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Estonia Mheshimiwa Toomas Hendrik Ilves na Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Kim, Profesa Kaushik alisema:
“Tuko katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia ya digitali inabadilisha maisha ya kijamii na kisiasa ya binadamu,” alisema Profesa Basu.
Aliongeza: “Chukulia takwimu hizi – kuna kiasi cha utafuta habari kwenye google kiasi cha bilioni 4.2 kwa siku moja, kila sekunde watu wanatuma tweet 6,000 na rekodi ilikuwa Agosti mwaka 2013 wakati zilipotumwa tweet 143,199 kwa sekunde wakati ilikuwa inaonyeshwa filamu moja ya sanaa.”
Aliongeza: “Mfumo wa uwekaji na utumaji pesa wa M-Pesa katika Kenya sasa unashindana na mifumo ya siku nyingi ya nchi matajiri duniani. Kila watu wazima 1,000 kuna akaunti 700 katika Kenya ikiwa ni ongezeko 103 kutoka mwaka 2013.”
“Jirani na Kenya kuna mfano mwingine wa mafanikio makubwa zaidi duniani katika nchi jirani ya Tanzania. Tanzania imewekeza sanakatika ICT na katika mfumo wa kuhamisha na kusambaza fedha. Sasa Tanzania ni soko kubwa zaidi duniani la kutuma fedha kwa njia ya simu,” alisema Profesa Kaushik.
Aliongeza: “Tanzania sasa ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma ya pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa njia ya simu. Hii ni mifano ambayo nchi zote duniani zinaweza kuiga kutoka Afrika.”
Wakati huo huo, Rais Kikwete leo, Jumanne, Septemba 28, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima wa Uholanzi, Mke wa Mfalme Willem-Alexander kuhusu jinsi gani ya kuzidi kuisaidia Tanzania kuongeza kasi yake katika kuboresha huduma za pesa kupitia ICT.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Septemba, 2015


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment