Image
Image

Wananchi wa Mtwara kunufaika na rasilimali za Gesi na Kilimo - MGHWIRA.


Mgombea urais kupitia chama cha ACT wazalendo Anna Mghwira ameahidi kuwa chama chake kitahakikisha raslimali zote zinazopatikana katika kila mkoa zinatambulika kikatiba ili wananchi wawe na uwezo wa kuhoji na kuzitumia kuboresha huduma katika mkoa husika.
Kauli hiyo ameitoa wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya mashujaa mjini mtwara,ambapo amesema kuwa serikali yake itahakikisha mkoa wa mtwara unanufaika na raslimali ya gesi sambamba na mazao ya kilimo yanayolimwa kwa wingi ili wananchi waweze kunufaika na ukuzaji wa uchumi katika maeneo yao.
Mh.Mghwira mapema akiwa katika wilaya ya newala,katika kijiji cha mnyambe jimbo la newala vijijini,ameelezwa na mgombea ubunge wa chama hicho Pilila Lawi Sijaona kuwa wilaya hiyo ina tatizo kubwa la maji licha ya kuwa na vyanzo kadhaa,ambapo ameahidi kumaliza tatizo hilo mara tu atakapopata ridhaa huku mgombea mwenza wa urais Hamad Yusuf akieleza kuwa ACT wazalendo itapanua na kuboresha bandari ya mtwara ili kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam.
Tayari mgombea urais wa ACT anna mghwira amekwishatembelea mikoa 13 kuomba kura.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment