Image
Image

Kiafya Korosho husaidia tatizo la moyo na mengine....

Korosho ni moja ya zao la biashara ambalo hupatikana sana Kusini mwa Tanzania, Mtwara, licha ya kwamba zao hili linafahamika sana kama zao la biashara, lakini bado zao hili lina faida kwa afya zetu pia.
Napenda kuchukua muda wako kwa sasa ili niweze kukuelekeza baadhi ya faidi za matumizi ya korosho kama ifuatavyo:
Matumizi ya korosho yanasifika sana kwa kuwa na uwezo wa kulinda afya ya moyo kutokana na kwamba korosha ndani yake inakirutubisho kiitwacho 'antioxidants'
Aidha korosho pia inasifika kwa kuwa na madini ya magnesium ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa na meno, lakini pia humsaidia mhusika anayependelea kutumia korosho kuwa na nafasi ndogo ya kupatwa na matatizo ya shinikizo la damu, hususani shinikizo la juu la damu.
Pia ulaji wa korosho husaidia sana kuimarisha afya ya usingizi na kumfanya mhusika kuacha kupata usingizi wa mang'amng'am na badala yake atajikuta akipata usingizi mzuri kabisa.
Mara nyingi kinamama wanaoingia kwenye kufungu hedhi 'menopause' wao huzongwa sana na tatizo la kukosa usingizi, hivyo wanashauriwa kutumia korosho ili kuepuka tatizo hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment