Image
Image

Ukibanwa na kikohozi fanya haya yafuatayo kukusaidia.

Kukohoa ni mojawapo ya njia ya kusafisha koo baadhi ya vitu ambavyo huweza kumfanya mtu kujisikia kutokuwa na amani kwenye koo lake, sasa pale anapokohoa ni kama anasafisha.
Lakini kukohoa pia huweza kusababishwa na maambukizi kwenye njia ya mfumo  wa hewa hapo ndipo sasa huwa tunasema mtu amepatwa na shida, huenda akawa anakohoa kwa sababu ya tatizo ya mzio au allergy ya baadhi ya vitu fulani fulani,
Moja ya dawa nzuri ya kukabiliana na shida hii ni matumizi ya asali na juisi ya limao, mtu mwenye tatizo la kukohoa mara kwa mara anashauriwa kupata mchanganyiko wa asali na limao kidogo ili kuondosha tatizo hilo.
Hata hivyo, endapo mhusika atakuwa anakohoa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo basi inashauriwa mhusika afike kwenye kituo cha afya kwa ajili ya vipimo zaidi ili kuweza kubaini endapo amepata maambukizi ya kifua kikuu na kuweza kuanza matibabu rasmi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment