Image
Image

Majabvi,amemjia juu mwamuzi,Israel Nkongo.


Kiungo wa kimataifa wa Simba,Mzimbabwe,Justice Majabvi,amemjia juu mwamuzi,Israel Nkongo, kwa kumtupia lawama kuwa ndiye aliyekuwa sababu kubwa kwa wao kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Yanga, wikiendi iliyopita.
Majabvi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza katika kikosi cha kwanza cha Simba kilichocheza na Yanga na kujikuta kikipokea kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.
 Majabvi amesema mwamuzi huyo aliwabeba  wapinzani wao Yanga kwa asilimia kubwa, jambo ambalo liliwaondoa kwenye mchezo.
 “Kiukweli sisi tulipoteza mchezo wetu kutokana na refa (Nkongo) kutuondolea umakini wetu baada ya kuonyesha mapenzi ya wazi kwa wapinzani wetu na kuwabeba bila ya sababu ya msingi.
“Nasema hayo kutokana na aina ya uchezeshaji wake ambapo alikuwa anawapa Yanga faulo hata kama siyo faulo na pia alitoa kadi za njano nyingi kwetu ili kuweza kutuzima na kuturudisha nyuma, naamini kama refa angekuwa ‘fea’ katika mchezo huu, basi Yanga wasingeweza kushinda,” alisema Majabvi ambaye ana bao moja mpaka sasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment