Image
Image

NEC –Wenye ulemavu watapiga kura kama wengine.


TUME ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema kuwa watu wote wenye ulemavu watapata nafasi ya kupiga kura kuchaguwa Diwani,Mbunge na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na kuwaandalia sehemu maalumu ya wao kupiga kura kwakuwa wanahaki za msingi kama watu wengine tofauti na ilivyokuwa inaelezwa kuwa watu hao hawataweza kupiga kura.
Kauli hiyo imetolewa hivi leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya watu wenye ulemavu na NEC mkutano huo wenye  lengo la kuwapatia uelewa kuelekea uchaguzi mkuu.
Kuhusu malalamiko yatolewayo na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa juu ya mchakato mzima wa uchaguzi kwa wengine kuona kama tume hiyo haitatenda haki kwenye uchaguzi wa mwaka huu Jaji Lubuva amedai kuwa hakuna haja ya kuanza kulalamikia pasipo kuwa na sababu kwani tume hiyo inajuwa wajibu wake na hivyo itatenda haki kwa kila mmoja kwa kuwa yenyewe ndio yenye dhamana hadi dakika ya mwisho.
Hata hivyo Tume hiyo ya uchaguzi imeendelea kusisitizia vyama vyote nya siasa kufuata maadili na kanuni wakati wa kampeni zao kwani hakitasita kukichulia hatua kali chama ambacho kitatumia mda mwingi jukwaani  kuwasema watu badala ya kunadi sera zake.
Aidha Lubuva amesema kuwa tiyari washaa vifikishia taarifa vyama vyote kufuata sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kuacha kutumia mda mwingi kujadili watu,bali tumewataka watangaze sera za chama husika na sio kutoa matusi jukwaani kwani kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kwakuwa wananchi wanataka sera si kuwasema watu wengine ama kuwakejeli.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment