Image
Image

Obama atoa ahadi ya kusaidia UN katika mipango ya maendeleo.


Rais Barack Obama asisitiza katika mkutano na Umoja wa Mataifa juu ya athari za maendeleo duniani kwa ajili ya njaa,umaskini na vita na kuahidi kuwa atajiunga nao katika harakati za kufanya maendeleo duniani.
Obama aliongea kuhusu mwongozo mpya wa wa kuondoa njaa na umaskini duniani kusema kuwa ajenda hiyo mpya ya kuleta maendeleo duniani itakuwa sio msaada bali ni njia ya uwekezaji bora ambao utaweza kukimu hali ya baadaye.
Obama alitoa utetezi mkubwa wa ajenda hiyo mpya itakayochukua muda wa miaka 15  ambao unatarajiwa kupata ufanisi wake wa matrilioni ya dola kutoka nchi kadhaa,makampuni na asasi za kiraia.
"Vita hutishia maendeleo ya nchi,na vita mara nyingi hutokana na utawala mbaya,"Obama alisema huku akigusia mgogoro wa wakimbizi mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia tangu vita vya pili vya dunia.
Viongozi kutoka Ufaransa,Japan na Uturuki pia walihutubia katika siku ya mwisho ya mkutano wa maendeleo unaofanywa kila mwaka kwa lengo ya kufanya mjadala wa ngazi za juu na kupa nchi tofauti kupitia viongozi wao kutoa maoni kwa upana kuhusu kufanya maendeleo duniani.
Hata hivyo taarifa ziliarifu kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin  hajaudhuria mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kwa muda wa muongo mmoja.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment