Image
Image

Umati wenye hasira na vurugu wawashambulia mashoga nchini Kenya.


Umati wenye hasira na vurugu wamekuwa wakiwashambulia mashoga mara kwa mara nchini Kenya licha ya kuwa waathiriwa wa mashambulizi hayo kupuuzwa na polisi wakipeleka malalamishi yao katika vituo vya sheria
Ushoga ni mwiko Kenya na karibu nchi zote barani Afrika,mashoga nchini Kenya hupewa adhabu ya kufungwa kwa muda wa miaka 14.
Limekuwa jambo la kawaida hasa Afrika ya mashariki kuwa na visa vya ukatili dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa mashoga na hata wakiwasilisha kesi zao polisi huonyesha kutojali kufuatilia kesi hizo.
Kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la kutetea haki za binadamu Kenya HRW,pwani ya Kenya kumekuwa na zaidi ya matukio 6 mwaka 2008 ya ukatili dhidi ya mashoga.
Mtafiti wa HRW Neela Ghoshal alisema kuwa viongozi wa kidini wa kikristo na kiislamu wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya uchochezi wa vurugu dhidi ya kundi hilo la watu.
Mnamo mwaka 2014 Uganda na Nigeria zilipitisha sheria ngumu dhidi ya mashoga ingawa baadaye sheria hiyo ilipinduliwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment