Image
Image

Serikali kufuta sheria kandamizi kwa wanawake.

TANZANIA imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake.
Badala yake itatunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia, yote katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania. Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.
Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa mwishoni mwa wiki na Rais Jakaya Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.
Rais Kikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa kwa pamoja na China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW).
Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia pamoja na kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa rasilimali fedha.
Rasilimali hizo zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Ajenda ya Kugharimia Maendeleo ya Addis Ababa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinatolewa pesa za kutekeleza mipango ya kitaifa na ya Serikali za Mitaa za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.
Itahakikisha pia utekelezaji wa uwakilishi wa uongozi wa asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume katika nafasi zote za maamuzi kwenye ngazi zote.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment