Image
Image

Tatizo la uhamiaji huko Ulaya limezidi kushika kasi.

Tatizo la uhamiaji huko Ulaya limezidi kushika kasi huku Denmark ikisimamisha usafiri wa
treni kuingia na kwenda Ujerumani.
Waziri Mkuu wa Denmark aidha amesema nguvu hazitatumiwa nchini humo dhidi ya wahamiaji
wanaojaribu kusafiri kupitia nchi yake kwenda kutafuta hifadhi nchini Sweden huku Umoja wa Ulaya ukiweka mgao wa wakambizi 120,000 kuchukuliwa na nchi wanachama.
Bwana Helle Thorning-Schmidt ametoa kauli hiyo baada ya Kampuni ya Taifa ya Reli nchini humo kusitisha huduma za reli za kutoka na kuingia Ujerumani baada ya kuendelea mzozo kati ya polisi na wahamiaji na kuzuia mamia ya wahamiaji wengine kutembea kwenye
barabara za magari kwa miguu kuelekea Sweden.
Nalo Jeshi la Hungary limeanza mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya kujiandaa kwa uwezekano wa baadaye kuwa na jukumu la kulinda mpaka wa kusini mwa nchi hiyo ili kuwazuia wahamiaji na wakimbizi kuingia nchini humo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment