Image
Image

Tuonyeshe ukomavu kidemokrasia.

WAKATI Kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiwa zinaelekea ukingoni, tunawakumbusha wafuasi wa vyama na wagombea mbalimbali kutambua kwamba uchaguzi huu ni fursa ya wananchi kufanya uamuzi wa nani wanataka kumchagua awe kiongozi wao.
Kampeni ni sehemu tu ya njia za kuwashawishi wananchi kuweza kukichagua na kukipa dhamana chama au mgombea wanayedhani anawafaa kwa mujibu wa mahitaji yao. Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mwisho wa kampeni ni Oktoba 24, saa 12 jioni. Baada ya hapo, ni wajibu wa raia waliojiandikisha kupiga kura kutekeleza haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Ni wazi kwamba ushawishi wa vyama vya siasa utaishia siku hiyo, na baada ya hapo litakuwa jukumu la NEC kuhesabu na kutangaza washindi katika nafasi mbalimbali zilizokuwa zikiwaniwa katika uchaguzi huo.
Katika kampeni zinazoendelea kuna viashiria vya baadhi ya vyama vya siasa kuandaa,ama kwa kujua au kutokujua,wafuasi wao kukataa matokeo ya uchaguzi.Tunapenda kuvikumbusha vyama hivi kujitahidi kuepuka kutengeneza mazingira hayo kwa wafuasi wao, kwa kuwa kufanya hivyo hata bila ushahidi wa namna gani wataibiwa kura, ni kutaka kuleta vurugu na kutishia kuvunja amani.
Ni wazi kwamba uchaguzi wa mwaka huu una ushindani mkubwa kuliko tulivyowahi kushuhudia katika uchaguzi wowote tangu tuanze mfumo wa vyama vingi.Bila shaka ushindani huu ni kielelezo cha kukua kwa demokrasia nchini kwetu.
Ukuaji huo wa demokrasia lazima uende sanjari na ukomavu wetu wa kisiasa, hasa kuonyesha kuvumiliana katika mazingira ya ushindani mkubwa kama tunayoyashuhudia sasa. Kielelezo cha kukua kwa demokrasia kisiwe tu katika ushindani tunaouona, kukua huku kunatakiwa kujidhihirishe pia katika kukubaliana na matokeo yatakayotokea hata kama hatutayapenda, lakini wenye nchi yao watakuwa wameamua hivyo.
Kwa sababu pamoja na kukua huko kwa demokrasia na ushindani tunaouona, hatimaye mshindi atakuwa mmoja tu. Hata kama kuna ushindani na mwamko wa kisiasa mkubwa kiasi gani, hatima yake itaishia kupata mshindi mmoja. Hili ndilo jambo ambalo vyama vyetu hasa vyenye ushindani mkubwa, vinaonyesha kutojiandaa nalo, na vivyo hivyo kwa wafuasi wao.
Ni wito wetu kwamba wakati tunafurahia ushindani huu unaoshiria kuimarika kwa demokrasia nchini, ni muhimu kwa viongozi wa vyama na wafuasi wao kuonyesha ukomavu huo wakati wa matokeo, kwamba kuna kushinda na kushindwa.
Tukifanya hivyo siyo tu tutakuwa tumeidhihirishia dunia ukomavu wa demokrasia nchini, bali tutakuwa tumefanikiwa kulinda na kutetea amani,umoja na mshikamano kama taifa.
WAKATI Kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiwa zinaelekea ukingoni, tunawakumbusha wafuasi wa vyama na wagombea mbalimbali kutambua kwamba uchaguzi huu ni fursa ya wananchi kufanya uamuzi wa nani wanataka kumchagua awe kiongozi wao.
Kampeni ni sehemu tu ya njia za kuwashawishi wananchi kuweza kukichagua na kukipa dhamana chama au mgombea wanayedhani anawafaa kwa mujibu wa mahitaji yao. Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mwisho wa kampeni ni Oktoba 24, saa 12 jioni. Baada ya hapo, ni wajibu wa raia waliojiandikisha kupiga kura kutekeleza haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Ni wazi kwamba ushawishi wa vyama vya siasa utaishia siku hiyo, na baada ya hapo litakuwa jukumu la NEC kuhesabu na kutangaza washindi katika nafasi mbalimbali zilizokuwa zikiwaniwa katika uchaguzi huo.
Katika kampeni zinazoendelea kuna viashiria vya baadhi ya vyama vya siasa kuandaa, ama kwa kujua au kutokujua, wafuasi wao kukataa matokeo ya uchaguzi. Tunapenda kuvikumbusha vyama hivi kujitahidi kuepuka kutengeneza mazingira hayo kwa wafuasi wao, kwa kuwa kufanya hivyo hata bila ushahidi wa namna gani wataibiwa kura, ni kutaka kuleta vurugu na kutishia kuvunja amani.
Ni wazi kwamba uchaguzi wa mwaka huu una ushindani mkubwa kuliko tulivyowahi kushuhudia katika uchaguzi wowote tangu tuanze mfumo wa vyama vingi. Bila shaka ushindani huu ni kielelezo cha kukua kwa demokrasia nchini kwetu.
Ukuaji huo wa demokrasia lazima uende sanjari na ukomavu wetu wa kisiasa, hasa kuonyesha kuvumiliana katika mazingira ya ushindani mkubwa kama tunayoyashuhudia sasa. Kielelezo cha kukua kwa demokrasia kisiwe tu katika ushindani tunaouona, kukua huku kunatakiwa kujidhihirishe pia katika kukubaliana na matokeo yatakayotokea hata kama hatutayapenda, lakini wenye nchi yao watakuwa wameamua hivyo.
Kwa sababu pamoja na kukua huko kwa demokrasia na ushindani tunaouona, hatimaye mshindi atakuwa mmoja tu. Hata kama kuna ushindani na mwamko wa kisiasa mkubwa kiasi gani, hatima yake itaishia kupata mshindi mmoja. Hili ndilo jambo ambalo vyama vyetu hasa vyenye ushindani mkubwa, vinaonyesha kutojiandaa nalo, na vivyo hivyo kwa wafuasi wao.
Ni wito wetu kwamba wakati tunafurahia ushindani huu unaoshiria kuimarika kwa demokrasia nchini, ni muhimu kwa viongozi wa vyama na wafuasi wao kuonyesha ukomavu huo wakati wa matokeo, kwamba kuna kushinda na kushindwa.
Tukifanya hivyo siyo tu tutakuwa tumeidhihirishia dunia ukomavu wa demokrasia nchini, bali tutakuwa tumefanikiwa kulinda na kutetea amani, umoja na mshikamano kama taifa. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/tuonyeshe-ukomavu-kidemokrasia#sthash.uLCVW3ej.dpuf

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment