Image
Image

Viongozi wa dini wawatahadharisha wananchi kuwa makini na viongozi wanaopenyeza chuki kuelekea uchaguzi mkuu.


Katika kudumisha hali ya amani na mshikamano uliopo hapa nchini wakati tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni,baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Kagera wamewatahadharisha watanzania kwa kuwataka wawe makini na wagombea wa nafasi za uongozi ambazo ni pamoja na urais, ubunge na udiwani ambao wanaoeneza siasa zenye viashiria vya kuwagawa  na kuchochea hali ya uvunjifu wa amani.
Tahadhari hiyo imetolewa leo kwa nyakati tofauti mjini bukoba na askofu msaidizi wa jimbo la kanisa katoriki la Bukoba,Methodius Kilaini na katibu mkuu wa baraza la waislamu (BAKWATA) wa mkoa wa Kagera Bashiru Kaboyo, ambao wanaelezea athari za siasa za udini, ukabila,chuki na kejeli zinazohubiriwa na baadhi ya wagombea zinavyohatarisha hali ya amani na mshikamano walionao watanzania.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Kagera,ali ame amesema chama hicho kwenye kampeni zake kitaendelea kuhuburi amani kwa kuwa amani inapovurugika inapelekea watu kukimbia nchi yao,naye Victor Sherejei ni katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  katika manispa ya bukoba anayetaja  mambo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini,huku augustine ulomi,kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera akiwatahadharisha viongozi watakaokiuka sheria za nchi kabla na baada ya uchaguzi mkuu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment