Image
Image

Tume ya uchaguzi nchini imetakiwa kufanya ziara za kimyakimya katika maeneo zinapofanyika kampeini huzo.


Wakati kampeini zikiendelea kushika kasi,Tume ya uchaguzi nchini imetakiwa kufanya ziara za kimyakimya katika maeneo zinapofanyika kampeini huzo, ili kubaini changamoto za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wagombea huko vijijini,na kuchukua hatua za makusudi,ikiwa ni pamoja na kubaini fununu zinazoenezwa juu ya watu wanaonunua vitambulisho  vya kupigia kura,kutoka kwa wananchi jambo ambalo litawakosesha haki ya kupiga kura.
Rai hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Bibi Magdalena Sakaya ambaye pia ni mgombea wa jimbo la kaliua mkoani Tabora,wakati akizungumzia changamoto za kampeini ambazo anakumbana nazo katika jimbo hilo ambapo amesema kuwa, bila tume kuzunguka wananchi wengi wanaweza wasipige kura. 
Suala la wananchi kupolwa vitambulisho vya mpiga kupigia kura limelalamikiwa na chama cha mapinduzi katika wilaya ya uyui mkoani humo,ambapo katibu wa chama hicho Bw.Inocent Namzaba amewataka wananchi kutorubunika kuvilinda kama mboni ya macho yao,huku mgombea ubunge jimbo la Tabora kasikazini akiwataka wananchi,kuunga mkono kaurimbiu yake ya siasa ni uchumi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment