Image
Image

Amri ya kutotembea usiku katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui yawekwa.

Amri ya kutotembea usiku imewekwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui
baada ya siku mbili za machafuko na mapigano kati ya makundi ya Wakristo na Waislamu.
Mapigano hayo yamesababisha watu 36 kupoteza maisha na wengine wapatao 30,000 kukimbia
makazi yao kufuatia mapigano yaliyozuka baada ya dereva Muislamu wa wa teksi kuuawa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana BAN KI-MOON ameonya kuwa Jamhuri ya Kati huenda ikarejea kwenye viwango vya machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka.
Rais wa mpito Bibi CATHERINE SAMBA-PANZA aliyekatisha kuhudhuria mkutano wa viongozi wa dunia mjini New York na kurejea nyumbani ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao na amekataa kujiuzulu.
Na katika hatua nyingine Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nayo imeamua kufunga mpaka
wake na Jamhuri ya Afrika ya Kati wenye urefu wa kilomita 1,750.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment