Image
Image

Kenya imepuuza onyo la Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya ICC.

Kenya imepuuza onyo la Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya ICC kutaka watu wake waache kujadili kesi ya mahakama hiyo inayomkabili Naibu Rais wa nchi hiyo Bwana WILLIAM RUTO na mwandishi wa habari JOSHUA ARAP SANG.
Jaji EBOE-OSUJI wa Mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo aliwaonya wanasiasa wa Kenya wanaodaiwa kuitukana mahakama hiyo hususani katika mikutano yao ya hadhara ya kutaka kuachiliwa kwao.
Hata hivyo akijibu kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku Kuu ya Mashujaa wa Kenya Rais UHURU KENYATTA aliwataka wale wanaowasakama Wakenya kuachana nao ili waunganishe nguvu zao katika kujenga nchi yao na kwamba wataendelea kutaka kuachiliwa kwa watuhumiwa wao.
Naibu wake Bwana RUTO na mwandishi wa habari JOSHUA ARAB SANG wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano yaliyosabisha vifo vya watu 1,300 huku wengine laki sita kukimbia makazi yao kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2007.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment