Image
Image

Toto Africans yaapa kuibana mbavu yanga licha ya ukubwa na jina lake.

Nawezekana isiwe ajabu sisimizi kumuua tembo! Huu ndiyo usemi unaoweza kuutumia kuelekea mchezo wa Yanga na Toto Africans baada ya Kocha Msaidizi wa Toto, John Tegete, kufunguka kuwa wanakutana na timu kubwa na ngumu lakini wanataka kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu huu.
Kocha huyo alisema kuwa, wanajua wanakutana na timu ambayo ipo vizuri lakini na wao wapo vizuri zaidi katika kupambana na kinachohitajika ni wachezaji wake kujiamini ili kuweza kufanikiwa kupata ushindi.
Timu hiyo tayari imecheza michezo saba msimu huu na ipo nafasi ya nane ikiwa na alama 10, huku Yanga wakiwa kileleni na pointi 16.
kocha huyo alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na hawana uchovu kwani wachezaji wake wote wapo fiti kwa ajili ya kupambana.
“Tunahitaji kuandika rekodi msimu huu kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga, ndiyo maana vijana wangu nimewapa mbinu ambazo zitaweza kuwasaidia katika mchezo huo ili kuweza kuibuka na ushindi.
“Hatuna majeruhi, wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya kupambana, hatuwaogopi Yanga kwani tulishawafunga kipindi cha nyuma tukiwa katika uwanja wetu wa nyumbani, hivyo ni jukumu letu kujituma na kuonyesha na sisi tunaweza mbele yao bila kujali rekodi zao,” alisema Tegete.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment