Image
Image

Pinda amewataka wawekezaji wa ndani katika sekta ya sukari kuhakikisha wanaimarisha viwanda.

Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amewataka wawekezaji wa ndani katika sekta ya sukari kuhakikisha wanaimarisha viwanda vyao kwa kuzalisha sukari kwa wingi kutokana na mahitaji ya bidhaa hiyo kuhitajika kwa watanzania wengi.
Waziri mkuu Pinda amesema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizindua nembo mpya ya kiwanda cha sukari cha Kilombero ambayo kwa sasa itakuwa na mwonekano mpya.
Amesema mahitaji ya sukari hapa nchini yameongezeka hivyo sasa wawekezaji wa ndani wana wajibu wa kuimarisha viwanda vyao kwa kuongeza uzalishaji zaidi kwa mujibu wa mahitaji katika soko la Tanzania.
Mh. Pinda amesema viwanda vya ndano vya sukari vinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba vinakidhi mahitaji ya watanzania kwa kuwa vinazalisha sukari iliyo bora na yenye viwango vinavyohitajika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment