Image
Image

LOWASSA aongoza watanzania kuuaga Mwili wa Dkt Makaidi katika viwanja vya Karimjee.


Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha National League for Democrasy-NLD- na mwenyekiti mwenza wa umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- Daktari Emmanuel Makaidi umeagwa leo katika viwanja vya Karimjee na kuzikwa katika makaburi ya Sinza jiji Dar es Salaam.
Katika ibada fupi ya kuuga mwili wa marehemu Daktari Emmanuel Makaidi iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.Bw. Edward Lowassa, wazii mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na makamu mwenyekiti wa CCM Bwana Philip Mangula, mchungaji wa kanisa TAG makumbusho Bwaba Davd Mwakwenda amewataka wanasiasa kuhacha kuombeana mabaya na kutakiana amani ili kuwa na taifa lenye baraka.
Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi ameiomba jamii kuhacha kuhusisha matukio ya vifo yanayoendele kujitokeza na harakati za kisiasa na kuwataka wanasiasa kutambua swala la amani ni la msingi hivyo taifa likiingia katika uchaguzi mkuu kwa amani litakuwa limemuenzi marehemu Daktari Emmanuel Makaidi. 
Akiongea kwa niaba ya umoja wa katiba ya wananchi Bwana James Mbatia amesema umoja huo umepata pengo kubwa kutokana na kifo cha mwenyekiti mwenza marehemu Dkt Makaidi kwa kuwa imekuwa ikituma taaluma yake ya sayansi ya siasa katika mipango yao, huku mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe akivita vyombo kisheria na mamlaka za kiserikali kutotumia nguvu ili kwezesha uchaguzi kuwa huru na amani kama njia ya kumuenzi marehemu Dkt Emmanuel Makaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment