Image
Image

Wabunge AU wahamasishwa kuridhia Mahakama ya Afrika.


Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), Jaji Augustino Ramadhani amewataka wabunge barani Afrika kuzishinikiza nchi zao kuridhia itifaki ya haki za binadamu iliyokubaliwa miaka 18 iliyopita.
Akihutubia Mkutano wa kwanza wa Kawada wa Kikao cha Nne cha Umoja wa Mabunge Barani Afrika, Midrand, Afrika Kusini juzi, Jaji Ramadhani ambaye pia ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania alisema kwamba nchi 25 bado haziridhia itifaki hiyo.
Alisema pia kwamba nchi 47 kati 54 wananchama wa Umoja wa Afrika (AU) hawakubali azimio linaloruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiseriakli (NGOs) kufungua kesi moja kwa moja mbele ya Mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania.
''Ninawasihi waheshimiwa kuziomba serikali za nchi zenu kuridhia Itifaki hiyo na kulikubali azimio linaloruhusu watu binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuja moja kwa moja mbele ya Mahakama ya Juu ya Haki za Binadamu barani,'' Jaji Ramadhani alisisitiza.
Tangu Itifaki hiyo ipitishwe mwaka 1988, ni nchi 29 tu ndizo zilizoridhia hadi sasa.
Nchi hizo ni pamoja na Algeria, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Ivory Coast, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) , Gabon, Gambia, Ghana, Kenya, Libya, Lesotho, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji ,Nigeria, Niger, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi, Senegal, Afrika Kusini,Tanzania, Togo and Tunisia.
 Hadi sasa ni nchi saba tu ambazo zimekubali azimio la kuruhusu watu binafsi na NGOs kufungua kesi mbele ya ACHPR. Nchi hizo ni pamoja na Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Malawi, Mali, Rwanda na Tanzania.
Tangu kuanzishwa kwake mahakama hiyo imeshashughulikia kesi 40.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment