Image
Image

Breaking News:Mgomo wa fukuta kiwanda cha urafiki wafanyakazi wadai maslahi yao.

Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki,Ubungo jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi kwa kushinikiza madai yao mbali mbali na nyongeza ya mishahara.
Mgomo wao unafuatia kushindwa kutekelezwa kwa agizo la mahakama ya kazi kwamba menejimenti ya kiwanda hicho na TUICO wakae kupitia majina ya zaidi ya watu elfu moja waliokuwa wanadai madai yao mbali mbali ikiwemo nyongeza za mishahara.

Akizungumzia malalamiko hayo Naibu Meneja Mkuu Msaidizi na Menejea wa Utawala wa kiwanda hicho Bwana MOSES SWAI amekiri kuwepo kwa madai ya msingi ya wafanyakazi hao na taratibu zilikuwa zinaendelea katika kutekeleza madai yao ili kumaliza tatizo hilo. 

Hata hivyo wafanyakazi hao wanasema wanaona viongozi wao wanasuasua kwa kutekeleza agizo hilo lililotolewa na mahakama mwaka 2008 na hivyo kuamua kuchukua hatua ya kugoma ili kushinikiza madai yao. 
Endelea kufuatilia taarifa zetu na Like Page yetu kwa habari zaidi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment