Kamati ya wabunge wote wa chama
cha mapinduzi CCM kwa kauli moja wamepitisha jina la mbunge wa kongwa mkoani
Dodoma Mh.Job Ndugai kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma
Mapema Leo.
Kuteuliwa
kwa jina la Ndugai ni baada wagombea wengine wawili kujitoa katika
kinyang"anyiro hicho cha Uspika ndani ya chama cha CCM .
Waliojitoa
katika mchakato huo wa kuchaguliwa katika nafasi ya Uspika ni pamoja na Mhe
Abdullah Ali Mwinyi na Dr Tulia Ackson Mwansasu hivyo kupisha nafasi hiyo
kwenda kwa Mh Job Ndugai.
Katibu wa itikadi na uenezi taifa Bwana Nape Nauye amesema kukamilika kwa uteuzi huo wa nafasi ya Uspika kunatoa
nafasi kwa wabunge wote wa CCM kumfanyia kampeni Mh.Job Ndugai ili aweze kuchaguliwa na wabunge wote katika mkutano wa bunge la kumi na moja
linalotarajiwa kuanza hapo kesho mjini Dodoma.


0 comments:
Post a Comment