Image
Image

Mhe.Kassim Majaliwa ala kiapo rasmi cha uwaziri mkuu wa Tanzania.

Rais Dakta JOHN MAGUFULI leo amemwapisha Mbunge wa Ruangwa, MAJALIWA KASIM MAJALIWA kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla hiyo fupi imefanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi wengine ni pamoja na Makamu wa Rais, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, Jaji Mkuu, Mheshimiwa MOHAMMED CHANDE OTHMAN, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JOB NDUGAI na Spika wa Baraza la Wawakilishi, PANDU AMEIR KIFICHO.
Leo alasiri Rais MAGUFULI anatarajiwa kulizindua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baada ya uzinduzi huo inatarajiwa kuwa Bunge litaahirishwa.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment