Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kuelekeza mazungumzo yao juu hatua
za pamoja na bara la Afrika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi, wakati
ambapo Slovenia imekuchukua uamuzi wa peke yake wa kufunga mpaka wake.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanapanga kupendekeza kwa viongozi wenzao wa
Afrika kiasi cha hadi yuro bilioni 3.6 kama msaada ili nchi hizo kwa
upande wake zihusike katika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi
wanaomimika kuingia nchi za Ulaya.
Mkutano huo wa aina yake unaowakusanya viongozi 50 kutoka mabara hayo
mawili unaonesha mwelekeo mpya katika nia ya Umoja wa Ulaya ya kuwa na
mkakati wa kushirikiana katika kupambana na mgogoro huo mkubwa ambao
haujapata kutokea tangu vita vya pilivya dunia.Hata hivyo hatua
iliychukuliwa na Slovenia ambayo ni mwanachama wa Umoja huo wa Ulaya ya
kufunga mpaka wake inaonesha kwa mara nyingine kuhusu kuwepo mgawanyiko
mkubwa ndani ya Umoja huo kuhusiana na jinsi ya kuushughulikia mgogoro
huo.
Jeshi la nchi hiyo lilianza hii leo kuweka senyeng'e katika mpaka wa
nchi hiyo na Croatia.Baada ya Hungary kufunga mpaka wake mwezi uliopita
Slovenia imejikuta kuwa njia kubwa katika eneo hilo la Balkan ya maelfu
ya wakimbizi wanaomiminika kutokea Ugiriki kila siku wakitumia njia
hatari ya kuvuka bahari kutoka Uturuki.
Afrika kupatiwa dola bilioni 3.6
Warasimu mjini Brusssles ambao wametia msukumo wa kufanyika mkutano huu
wa Malta wanapinga hatua za kufungwa mipaka wakisema ni hatua
inayochangia tu kuwafanya wakimbizi watafute njia nyingine na wakati
huohuo inahujumu juhudi za kupatikana suluhisho la pamoja.
Kwahivyo katika mkutano huo wa siku mbili Umoja wa Ulaya unataka
kuwashawishi viongozi wa nchi za Afrika kukubali kuchukua dola bilioni
3.6 kwa sharti kwamba zitakuwa tayari kuwapokea wahamiaji wanaozikimbia
nchi za bara hilo kutokana na hali ngumu ya kiuchum.Hata hivyo hadi sasa
nchi hizo za kiafrika zinaonesha kutokuwa tayari kuingia kwenye mwafaka
huo kwa kuhofia kupoteza mabilioni ya dolla zinazoingia kwenye nchi
hizo kupitia fedha zinazotumwa na wanachi wao wanaofanya kazi nchi za
nje.
Nchi za Ulaya zinalenga hasa kuimarisha ushirikiano wake na nchi za
Afrika kuwalinda wakimbizi,kuwarudisha nyumbani wahamiaji wa mara kwa
mara pamoja na kukomesha biashara ya kuwapitisha kimagendo wakimbizi hao
wakati pia ikiwapa nafasi waafrika kutanua njia za kisheria za
uhamiaji. Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Donald Tusk fedha
zitakazotolewa kwa Afrika zitasaidia kuzifanya pande hizo mbili Afrika
na Ulaya kushirikiana kuweka mustakabali mzuri kwa watu wa Afrika katika
wakati ambapo vijana barani humo wamekuwa mara nyingi wanajikuta
wakilazimika kuchagua kati ya kubakia bila ajira au kuingia kwenye
makundi ya siasa kali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment