Image
Image

MSD kuweka nembo ya serikali kwenye dawa zake.

Serikali imesema kuwa itahakikisha dawa katika Mahospitali na Vituo vya afya zinapatikana kwa wakati kama ambavyo ahadi ya Rais Dkt. Magufuli aliyokuwa akiitoa katika kampeni zake, sasa ni hatua ya utekelezaji wa ahadi hii kwa wananchi.
Katika kulitekeleza hilo, Mkurugenzi  Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu aliagizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Donan Mmbando kwa niaba ya Rais, kuhakikisha kuwa dawa zote za Serikali zinakuwa na utambulisho maalum ili endapo zikikutwa zipo katika maduka ya dawa binafsi, basi hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wamiliki wa maduka hayo.
Ikumbukwe, MSD inahudumia hospitali za Serikali tu na vituo vyake na kamwe dawa ambazo husambazwa na MSD hazipaswi kuuzwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi, Hivyo ni kosa la jinai kwa dawa za Serikali kukutwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Ameeleza Mkurugenzi wa MSD.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa, MSD itafungua maduka ya dawa makubwa karibu na mahospitali ya Serikali ili kurahisisha zaidi upatikanaji wa madawa kwa urahisi ikiwa ni kusambaza madawa hayo kote nchini katika vituo vya afya kwa wakati, ili wananchi wote wenye uhitaji wa madawa waweze kupata bila tabu yoyote ile.
Kwa kuhitimisha, Mkurugenzi huyo ametoa namba maalum na itabandikwa kwenye vituo vya afya na mahospitali yote ya serikali kwa dhumuni moja la msingi ambalo ni endapo mwananchi yeyote atapata tabu katika kupatiwa dawa, basi atumie namba hiyo kutoa taarifa MSD na kupiga ni BURE kabisa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment