Image
Image

MSD yaidai Serikali zaidi ya deni la shilingi bilioni 102.

Deni ambalo Bohari Kuu ya Dawa (MSD) linaidai serikali limezidi kuongezeka kutoka Sh. bilioni 102 mwaka jana na kufikia Sh. bilioni 114 mwaka huu. Kiasi hicho ni ongezeko la Sh. bilioni 12 lililotokana na gharama  ya utoaji wa mizigo bandarini, usambazaji wa dawa na vifaa tiba, madeni ya hospitali, vituo vya afya na zahanati.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Lauren Bwanakunu, fedha hizo zinapaswa kulipwa na Hazina kupitia Wizara ya  Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza na Tambarare Halisi liiyotaka kujua kuhusiana na deni hilo, Bwanakunu alisema kutokana na deni hilo MSD imeshindwa kuwalipa wazabuni wake wanaowapelekea dawa ambao wamegoma kuendelea kutoa huduma hiyo hadi pale watakapolipwa fedha zao.  

Alisema pia wazabuni wengine wanaowategemea kuwapelekea dawa wamesimamisha huduma kutokana na mikataba waliyokuwa nayo kumalizika. “Hali hii imesababisha MSD kushindwa kukidhi manunuzi ya dawa kama yalivyo matarajio ya mwaka huu wa fedha, jitihada zinaendelea hata hivyo tunaweza kupata fedha kidogo ndani ya muda mfupi kulingana na uwezo wa serikali na sisi tuweze kuwalipa wazabuni kuwapa imani,” alisema.

 Bwanakunu alisema kwa taratibu za MSD, kila hospitali, zahanati au kituo cha afya huagiza dawa mara nne kwa mwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu. Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donald Mbando, alisema hadi sasa serikali imeshalipa deni inalodaiwa na MSD Sh. bilioni 42 katika mwaka wa fedha uliopita.

Alisema serikali ipo katika mikakati ya kulipunguza zaidi kwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha katika mwaka wa fedha 2015/16.

Hata hivyo, alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya uhakiki wa deni hilo na kutaja deni kamili kuwa ni Sh. bilioni 54 na kwamba serikali italipa deni hilo kwa kufuata taratibu na taarifa ya CAG na siyo kiasi cha deni kinachoelezwa na MSD kuwa ni Sh. bilioni 114.

Taarifa zilizowahi kuthibitishwa na aliyewahi kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Seleman Rashid wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii mwaka jana na kuripotiwa  na gazeti hili zilionyesha kuwa MSD inaidai serikali Sh. bilioni 102.

Alieleza kuwa baada ya MSD kuona kuwa madeni yanazidi kulimbikizwa huku kasi ya serikali ikiwa ndogo katika kulipa, iliamua kusitisha huduma zake kwa serikali, lengo likiwa ni kushinikiza walipwe fedha hizo ili waendelee kutekeleza majukumu yao kama yalivyoanishwa katika Sheria Namba 3 ya kuanzishwa kwake mwaka 1993.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment