Image
Image

Mwili wa Alphonce Mawazo waagwa kishujaa jijini Mwanza*Mtoto wa Marehemu awaliza waombolezaji.


Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza,wakiongozwa na mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) Mh. Freeman Mbowe wameuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita Alphonce Mawazo,huku baadhi ya viongozi wa chama hicho,wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu wakilitaka jeshi la polisi mkoani Geita kuhakikisha watu waliohusika na mauaji ya kiongozi huyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja.

Tukio la kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza limetanguliwa na ibada iliyoongozwa na mchungaji Bernard Swai wa kanisa la Winners.

Fredrick Sumaye, waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ), Mh. Edward Lowassa wakatoa angalizo kwa jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linatenda haki katika kushughulikia kifo cha marehemu Alphonce Mawazo.


Mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh. Freeman Mbowe naye akatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Alphonce Mawazo, aliyeuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha Katoro wilayani Geita.

Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo tayari umewasili mjini Geita ambako utalala usiku huu ili kutoa nafasi kwa wananchi wa mkoa huo kutoa heshima zao za mwisho siku ya jumapili asubuhi Novemba 29, kabla ya kupelekwa nyumbani kwao katika kijiji cha Chikobe kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya jumatatu Novemba 30.
Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo,Precious Mawazo mwenye umri wa miaka tisa akatokea mbele ya halaiki kuelezea majonzi ya kufiwa na baba yake.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment