Image
Image

Nkunga:Waajiri zingatieni haya kwa wafanyakazi wenu.


Na.Mwandishi Wetu,Morogoro.
Imeelezwa kuwa ili kuleta ufanisi mzuri kazini,waajiri na waajiriwa wanatakiwa kutekeleza kisheria yale yote wanayokubaliana katika utendaji wao wa kazi.

Akizungumza na Tambarare Halisi Afisa Mwandamizi wa kazi na Ajira mkoa wa Morogoro JULIUS NKUNGA amesema ili kazi iweze kufanyika  kwa ufanisi mzuri ,kwa haki na uhuru ni lazima waajiri na waajiriwa wote kufuata kikamilifu sheria zinazowapasa.

NKUNGA ameongeza  kuwa kuna baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo ambazo ni pamoja na uhaba wa fedha na ikizingatiwa katika kitengo chao wanatakiwa kutoa huduma kwa wilaya sita hivyo wanaiomba serikali kuliangalia vyema suala hili hasa katika utengwaji wa bajeti.

Aidha NKUNGA amesema katika kitengo kinachojishughulisha na kusimamia sheria za kazi kwa ujumla wanajitahidi kutoa elimu kwa waajiri na waajiriwa katika kuhakikisha kila mmoja anazifuata sheria na hatimaye kuwa na  utendaji mzuri wa kazi.

Hata hivyoElimu hizo hutolewa kwa njia ya semina na warsha mbalimbali baada ya kuwepo kwa malalamiko yanayohusiana na matatizo waliyoyapokea ya waajiri na waajiriwa ili kutoa ufumbuzi .


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment