Mamlaka ya mapato -TRA imesema mpaka mwishoni mwa
mwezi Oktoba ilikuwa imefikia asilimia
97.6 ya malengo waliyokuwa wamewekewa na serikali ya kukusanya kodi kwa mwaka huu ambapo walikuwa wamekusanya shilingi trilioni 12.3.
Kamishina mkuu wa mamlaka hiyo Rished Dade amewaambia
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika miezi ya Novemba na Desemba
wanatumai watakuwa wamekusanya kodi zaidi ya asilimia mia moja ya lengo
walilokuwa wamekewa na serikali.
Kuhusiana na agizo la rais Dr.John Magufuli kuziba
mianya ya ukwepaji kodi na kuwabaini wakwepa kodi ,kamishina Bade amesema
mamlaka yake itahakikisha inalitekeleza
hilo na kuwa sasa imeendelea na mkakati wake wa kukutana na wadau mbalimbali wa
masuala ya kodi kuzungumza nao juu ya
kulifanikisha hilo.
Nao moja kati ya wadau wakuu wa ulipaji kodi nchini mawakala wa forodha-TAFFA
kupitia mwenyekiti wao Steven Ngatunga
amesema wapo tiyari wao na taasisi
zingine za kibiashara nchini kushirikiana TRA katika kuibaini mianya ya ulipaji
kodi ili kumuwezesha Dr.Magufuli na serikali ya awamu ya tano kutimiza malengo yake.


0 comments:
Post a Comment