Image
Image

Wafugaji wamuomba Rais.Magufuli akomeshe migogoro ya wakulima na wafugaji.

Wafugaji wilayani Tunduru wamemuomba Rais  JOHN MAGUFULI akomeshe migogoro kati ya wafugaji na wakulima nchini  ambayo imepoteza maisha ya wafugaji na wakulima na aweke usawa  baina ya wananchi na wawekezaji.
Wafugaji hao wenye zaidi ya ng'ombe elfu thelathini na wanne walioingia nao kutoka bonde la Ihefu mkoani Mbeya, wametoa ombi hilo katika kijiji cha Kidodoma.
Wamesema pamoja na kumpongeza Dakta JOHN MAGUFULI kwa kuchaguliwa kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemuombaawatambue wafugaji kwa sababu wanachangia pato taifa kupitia mifugo  yao ingawa hawathaminiwi  na mifugo yao inaonekana ni haramu.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa kijiji cha Kidodoma  Bwana ALIFA  MAKUNGANYA  amesema halmashauri hiyo ina uhusiano mazuri na wafugaji hao ambao wanachangia fedha katika  maendeleo ya kijiji.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment