Image
Image

Wananchi na viongozi Mkoani Arusha wafanya zoezi la usafi kukabiliana na Kipindupindu.



Ugonjwa  wa  Kipindupindu   unaendelea  kutishia  maisha  ya  wananchi  wa  mkoa  wa  arusha hali  ambayo  imewalazimu  viongozi  wa  mkoa  huo  na  wananchi  wakiwemo  raia  wa  kigeni  kuendesha  zoezi  la  usafi  wa  mazingira  katika  maeneo  mbalimbali   ya kama  sehemu  ya  kampeni  za  kukabiliana  na  janga  hilo

Akizungumza  baada  ya  kuongoza  zoezi  hilo  lililoanza  alfajiri  kaimu  mkuu  wa  mkoa   wa  arusha   Bw.Fadhili Nkurl  amesema  zoezi  hilo  ni  endelevu  na ni wajibu  wa  kila  mmoja kufanya usafi  katika eneo  lake  na amewataka  watendaji   wa  jiji  kuhakikisha  kuwa  yeyote  anayekaidi   anachukuliwa  hatua.

Bw.Nkurl pia  amemtaka  mkurugenzi  wa jiji kuhakikisha  kuwa  watendaji  wanaosimamia  idara ya usafi  wanatimiza  wajibu  wao   wakiwemo   wanaoshughulikia  uzoaji  wa  taka  ambao  wamekuwa  wakilalamikiwa  na  wananchi.

Kwa  upande  wao  watendaji  wa  baadhi  ya  taasisi  wakiwemo  Dr. Christopher Nzela kutoka  chama  cha  msalaba  mwekundu  wamesema udhibiti wa  ugonjwa  wa  kipindupindu  ni jambo  linalowezekana  tena  lisilo  na  gharama  kinachohitajika  ni  kila  mmoja  akitimiza  wajibu   wake.

Iidadi  ya wagonjwa  wa  kipindupindu  katika  mkoa wa  arusha  imekuwa  ikionhezeka  na  kupungua  na  hadi  sasa  wagon jwa  watano  wamelazwa  katika  kituo  cha afya  cha  levolosi  wakiendelea  na  matibabu  na  kutokana  na  kukithiri  kwa  uchafu  mkoa  wa  arusha  umetenga  siku  ya  jumamosi  ya  mwisho  wa  mwezi  kuwa  ni  ya  kufanya usafi  wa  jumla.





Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment