Wakizungumza
na East Africa Radio wakiwa nje ya ofisi hiyo, wamesema mara kadhaa
wamekuwa wakitekeleza bila mafanikio, maagizo wanayopewa na wahusika kwa
kuwapangia tarehe za kupatiwa vyeti hivyo lakini inashindikana kutokana
na ofisi kuwa inafungwa kila wanapofika na kukosa mtu wa kuwahudumia.
Wamesema, ofisi hiyo imeanza kufungwa tangu mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika mwezi Oktoba, kutokana na muhusika kuamua kujiingiza katika siasa.
Kwa upande wake, afisa tawala wa wilaya ya Mtwara, ambako ndiko kuna ofisi hiyo, Edith Shayo, amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao na kusema kuwa mara kadhaa anajitahidi kutoka na kuwaeleza changamoto walizo nazo zinazosababisha ofisi kufungwa na wao kukosa huduma.

0 comments:
Post a Comment