Image
Image

Sababu ya wagonjwa kulala chini katika hospitali ya Muhimbili yabainika.


Uhaba wa majengo ya kulaza wagonjwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ndiyo sababu ya idadi kubwa ya wagonjwa kulala chini na wengine kulazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja hasa wodi ya wazazi kwani kwa zaidi ya miaka hamsini haujawahi kufanyika upanuzi wa wodi.

Afisa uhusiano wa hospitali ya muhimbili bw aminieli eligaeshi amebainisha hayo alipokuwa akipokea msaada wa vitanda 30 na magodoro yake vya kulaza wagonjwa ambapo amesema suala la msongamano haliwezi kuepikika hadi majengo yatakapoongezwa kwani idadi ya wagonjwa inaongezeka kila siku ilihali majengo ni yale yale.

Naye mwakilishi wa mkurugenzi wa idara ya uuguzi na ubora wa hospitali hiyo bi mariana makanga akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo mbali na kushukuru amesema itawapunguzia wauguzi adha ya kuhudumia mgonjwa akiwa amelala chini.

Kwa upande wake msamaria aliyetoa msaada huo amesema ni baada ya rais dk john magufuli kutembelea hospitali hiyo na kubaini changamoto zinazoikabili hivyo naye akaguswa kusaidia huku akitoa wito kwa wengine.

Akizungumzia suala la mashine ya MRI kufanyakazi siku moja baada ya rais kutembelea hospitali hiyo hali iliyozua maswali mengi kwa wananchi na wagonjwa bw eligaeshi amesema.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment