Image
Image

Vigogo 18 wa CCM wachuana kuchukua fomu za Uspika Lumumba jijini Dar es Salaam.


Wagombea 18 wa nafasi ya kiti cha Spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM wamejitokeza na kuchukuwa fomu huku baadhi ya waliokosa ubunge nao wakijaribu bahati yao kwa mara nyingine kupitia kiti hicho akiwemo Didas Masaburi.

Wakichukua fomu katika ofisi ndogo za ccm zilizopo lumumba jijini Dar es Salaam baadhi ya wagombea hao wameelezea baadhi ya mambo yaliyowasukuma kugombea nafasi hiyo nyeti kwa taifa.

Katibu wa idara ya oganizesheni wa CCM Dk.Mohamed Seif Khatibu mbali na kuwataja makada waliokwisha chukuwa fomu amesema wagombea 16 siyo wabunge na wagombea wawili ni wabunge na kwamba nafasi bado ziko wazi kwa kila kada anayeona anakidhi kushika wadhifa huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment