Image
Image

Watu 36 katika kila watu 100 ya Watanzania ndio wanaopata huduma ya maji ya bomba nchini.

Watu  36 tu katika kila watu 100 ya Watanzania, ambayo ni sawa na asilimia 36,  ndiyo wanaopata huduma ya  maji ya bomba  nchini .
Wengine wengi  hutegemea maji ya visima au maji ya kwenye madimbwi ambayo kwa ujumla siyo safi na salama  na kwamba k atika suala la upatikanaji wa maji, tofauti kati ya wakazi wa mijini na vijijini ni kubw a.
Matokeo hayo yametolewa na  taasisi ya  TWAWEZA kwenye muhutasari wa utafiti wenye jina la Nusu Nusu  yaliyotokana na m aoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa maji safi.
Muhutasari huu umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu za mikononi.
Licha ya kuanzishwa kwa Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa na ku k a milika  kwa kipindi cha Malengo ya Maendeleo ya Milenia,upatikanaji wa maji haujabadilika katika kipindi cha mwaka jana.
Matokeo yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,852 wa Tanzania Bara kati ya tarehe 9 Septemba na 26 Septemba  mwaka huu na  Zanzibar haikuhusishwa kwenye matokeo hay o .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment