Rais wa shirikisho la kandanda duniani Fifa Sepp
Blater ambae amesimamishwa kwa muda wa siku tisini kutojihusisha na soka,
ametaka kifungo hicho alichofungiwa kwa muda cha kutojihusisha na maswala yote
ya soka kufutwa.
Mwanasheria wa kiongozi huyu wa juu wa zamani
shirikisho hilo la soka Richard Cullen, amesema ushahidi alionyesha kwamba
Blatter alipokuwa ndani ya Fifa hakuwahi kukiuka maadili ya chama hicho.
Wakili huyu alikuwa akizungumza baada ya jopo la
maadili la Fifa kusema uchunguzi umefungwa.
Blatter alifungiwa kwa siku 90 kuanzia mwezi oktoba
kwa tuhuma za malipo ya dola milioni mbili dhidi ya raisi wa Uefa Michel
Platini, ambae pia amefungiwa kwa sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment