Mwanasheria mkuu wa zamani wa Tanzania, Jaji Mark
Bomani, anasema hali ya kisiasa visiwani Zanzibar inatishia mustakabali wa eneo
hilo na kama uchaguzi mpya utafanyika basi lazima usimamiwe na jopo maalumu la
wataalamu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, mwanasheria huyo amesema kuwa kile kinachoendelea visiwani humo
hakiashirii picha njema hivyo akashauri kuchukuliwa kwa hatua za kibusara kwa
ajili ya kukwamua mzozo huo.
Ikiwa ni kauli yake ya kwanza tangu kufutwa kwa
uchaguzi huo miezi miwili iliyopita, Jaji Bomani amesema kuwa iwapo hali hiyo
itaachwa iendelee inaweza kusababisha madhara makubwa jambo ambalo linaweza
kuirudisha nyuma Zanzibar.
Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na ripoti kwamba
viongozi wa pande zote CCM na CUF wamekuwa wakikutana mara kwa mara Ikulu ya
Zanzibar katika kile kinachoelezwa kuwa ni jitihada za kujaribu kutanzua hali
hiyo.
Tangu kuanza kwa vikao hivyo hakuna upande uliokuwa
tayari kuelezea maendeleo yaliyofikiwa huku baadhi ya maofisa wa CUF
wakiendelea kusisitiza haja ya kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huo ambao
ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha
Ama mwanasheria huyo ambaye amekuwa akitokeza
mara kwa mara kutoa maoni yake pindi kunapojitokeza utata katika masuala ya
kitaifa, amesema kuwa pande zote mbili yaani CCM na CUF bado haziaminiani hivyo
iwapo hata kutarudiwa kwa uchaguzi huo hali itajirudia ile ile.
Kwa maana hiyo alitaka kuundwa kwa jopo maalumu la wataalamu wa mambo ikiwamo kutoka jumuiya ya kimataifa ili kushughulikia uchaguzi mwingine. CCM Zanzibar yaendelea kung'ang'ania uchaguzi.
Kwa maana hiyo alitaka kuundwa kwa jopo maalumu la wataalamu wa mambo ikiwamo kutoka jumuiya ya kimataifa ili kushughulikia uchaguzi mwingine. CCM Zanzibar yaendelea kung'ang'ania uchaguzi.
Hayo yakiarifiwa, visiwani Zanzibar hali
imeendelea kuwa ya taharuki kutokana na kutojuilikana hasa hatima ya mzozo huu.
Hivi leo, mitandao ya kijamii ilizagaa taarifa za baadhi ya viongozi wa CCM
kujitayarisha kuchukuwa hatua za kushinikiza kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi
mpya, licha ya mazungumzo yanayoendelea.
Akizungumza na DW kwa njia ya simu akiwa mjini
Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai, alisema pamoja na kuwa
wanayaunga mkono mazungumzo yanayofanyika kuukwamua mkwamo wa kisiasa na
kisheria uliopo "bado lazima sheria zifuatwe".
CCM inaunga mkono tamko la kufutwa kwa uchaguzi la
hapo tarehe 28 Oktoba 2015 na inasisitiza kuwa lilitolewa kwa mujibu wa sheria
za nchi, hoja inayopingwa vikali na wanasheria mbalimbali nchini Tanzania.
Kufutwa kwa uchaguzi huo ambao ni tukio la
kihistoria kwa siasa za Tanzania kulikosolewa pia na wawakilishi kadhaa wa
jumuiya za kimataifa ikiwamo zile zilizotuma waangalizi wake katika uchaguzi
huo.
Marekani, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na taasisi za kiraia ni baadhi ya wale walijitokeza na mapema kulaani hatua hiyo wakitaka matakwa ya wananchi wa Zanzibar yasikilizwe.
Uchaguzi wa Zanzibar mara zote umekuwa ukiibua masuala tete na wakati mwingine kuchafua hali ya kisiasa.
Majadiliano ya mwaka 2009 kati ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Karume, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kiasi kikubwa yalifanikiwa kuzika hali ya uhasama na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa serikali ambayo kwa sasa iko majaribuni kutokana na mvutano huu unaoendelea.

0 comments:
Post a Comment