Baada ya Zoezi la bomoabomoa awamu ya pili kuwakumba
wakazi wa Bonde la Mto msimbazi na kulalamikia kuwa hawakupewa taarifa yeyote
juu ya zoezi hili,Hatimaye Afisa Mipango-miji Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya
Makazi, CHARLES MKALAWA amelitolea ufafanuzi na kusema kuwa eneo ambalo
bomoabomoa inaendelea la Bonde la Mto Msimbazi limeshatangazwa tangu mwaka
1979 kuwa ni eneo hatarishi na kwamba ni kinyume cha sheria kwa mtu
yeyote kufanya makazi au kufanya shughuli yoyote ndani ya eneo hilo.
Amesema zoezi hilo limefuata sheria na limewahusisha
wote wanaohusika wakiwemo Maafisa wa Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Ardhi na
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa pia analifahamu zoezi hilo.
Kwani bomoa bomoa hii ya awamu ya pili
kufanyika jijini kwa kudhuru nyumba zilizojengwa kwenye maeneo
yasiyoruhusiwa kufuatia bomoa bomoa ya kwanza iliyofanyika mwezi uliopita
maeneo ya Mbezi Beach na kusimamiwa na Wizara ya Ardhi na Maeneleo ya Makazi
inaendelea hadi pale watakapo kamilisha agizo la serikali.
0 comments:
Post a Comment