Uongozi wa klabu ya Yanga,umetangaza kumsimamisha
Haruna Niyonzima kwa muda usiojulikana.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema
Niyonzima amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.
“Amekuwa akifanya mambo ambayo yanaonyesha wazi ni
ukiukaji mkataba hasa katika masuala ya utendaji.
“Lakini amekuwa akionyesha utovu wa nidhamu. Kwani licha
ya kukaa naye pamoja na kuzungumza naye kuhusiana na hali hiyo bado amerudia.
“Tulikaa naye Novemba 4, ilikuwa pale Protea Hotel.
Tukajadiliana na mwisho akaomba msamaha na kuahidi asingerudia tabia hiyo ya
kuwa mchelewaji kurejea kazini kila anapokwenda Rwanda.
“Lakini amerudia safari hii, tena akijua wazi
alijiunga na timu ya taifa ya Rwanda bila taarifa kwa klabu. Halafu baada ya
fainali ya Cecafa akazima simu kabisa,” alisema Dk Tiboroha.
0 comments:
Post a Comment