Chama cha siasa za mrengo wa kulia nchini Ufaransa, National Front - FN,
kimeshindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa majimbo nchini humo,
bila kupata hata jimbo moja .
Hayo ni licha ya kutawala katika duru ya kwanza mwishoni mwa wiki
iliyopita. Huku uchaguzi wa rais ukitarajiwa mwaka wa 2017, chama cha FN
kinachopinga uhamiaji kilitarajia kuwa uchaguzi huu wa majimbo
ungetumika kama mwanzo wa safari ya kiongozi wake Marine Le Pen.
Licha ya FN kuwa na matokeo mazuri katika kura za kitaifa, Le Pen
aliangushwa na upinzani wa mrengo wa kulia katika jimbo la
Nord-Pas-de-Calais-Picardie baada ya chama tawala cha Kisioshaliti
kujiondoa katika kinyang'anyiro kabla ya duru ya pili. Le Pen alielezea
matumaini licha ya kushindwa. Le Pen amesema "Matokeo ya mwanzo thabiti
yalipatikana tangu raundi ya kwanza na kusababisha kutokomezwa moja kwa
moja toka ngome zao za kaskazini na kusini mashariki chama cha
Kisoshialisti cha eneo hilo, ambacho hakikuwa na faida kwa yeyote".
Le Pen amesema ikilinganishwa na uchaguzi wa mwisho wa majimbo mwaka
wa 2010, orodha zao zimepata kura zaidi kutoka asilimia 9.17 hadi
asilimia 30 katika duru ya pili, ikiwa ni baada ya miaka mitano pekee.
Mpwawe aliye na umri wa miaka 26 Marion Marechal-Le Pen pia alishindwa
katika jimbo la kusini ambalo lina pia maeneo ya kifahari kama vile Cote
d'Azur, licha ya kutawala katika duru ya kwanza wiki iliyopita
Chama hicho kilishinda kura katika majimbo sita kati ya 13 mnamo Desemba
6, kikiwa na asilimia 28 ya mgao wa kura kitaifa, iliyochochewa na
ghadhabu kuhusiana na uchumi unaoyumba na wasiwasi uliozuka kufuatia
mashambulizi ya kigaidi ya mwezi uliopita mjini Paris yaliyowauwa watu
130.
Lakini mwezi mmoja baada ya mashambulizi hayo, wapiga kura walijitokeza
kwa wingi – karibu asilimia 58 walishiriki, ikiwa ni juu kutoka asilimia
50 iliyojitokeza katika duru ya kwanza – na kwa mara nyingine
wakakiangusha FN katika mkondo wa mwisho. Waziri Mkuu Msoshialisti
Manuel Valls ameonya kuwa licha ya matokeo hayo "kitisho cha chama cha
siasa za mrengo wa kulia cha FN bado hakijaondolewa kabisa".
Sarkozy, kiongozi wa chama cha Republican amewapongeza wapiga kura
lakini naye akasema kuwa onyo lililojitokeza katika duru ya kwanza
halipaswi kusahaulika. "Sasa tunapaswa kuchukua muda kwa ajili ya
majadiliano ya kina kuhusu kinachowapa wasiwasi Wafaransa – ambao
wanatarajia majibu imara na ya kweli – na ambayo tunawajibikia.
Ninatafakari kuhusu Ulaya, sera ya uchumi, ukosefu mkubwa wa ajira,
usalama wetu, namna elimu ya watoto inavyoendeshwa, na utambulisho
wetu".
Chama tawala cha Kisoshialisti cha Rais Francois Hollande kilishinda
katika majimbo matano, huku muungano wa siasa za wastani za mrengo wa
kulia wa mtangulizi wake Nicolas Sarkozy kikinyakua majimbo saba. Chama
cha Wazalendo kilishinda jimbo la Corsica.
Mojawapo ya matokeo ya kushangaza katika uchaguzi huo ni katika jimbo la
Paris, ambao ulihama kutoka mrengo wa kushoto na kwenda wa kulia kwa
mara ya kwanza katika miaka 17.
Matokeo ya mwisho yalionyesha kuwa Le Pen alishinda karibu asilimia 42
dhidi ya karibu asilimia 58 ya mpinzani wake wa mrengo wa kulia Xavier
Bertrand katika upande wa kaskazini wenye matatizo ya kichumi.
Katika hotuba yenye jazba baada ya vituo vya kura kufungwa, Le Pen alisema hakuna kitakachowazuia sasa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment