Image
Image

CUF yajibu mapigo kwa CCM yasema haitorudia uchaguzi msimamo wao upo palepale.



Wazanzibari wanaendelea kuwa njiapanda juu ya mgogoro wa kisiasa visiwani humo  baada ya chama cha wananchi- CUF- kupingana na kauli ya chama cha mapinduzi na kudai hakuna marudio ya uchaguzi na kuwataka wazanzibar kusubiri matokeo ya mazungumzo ya viongozi wa juu serikalini.
Kauli hiyo ya CUF  imetolewa na kaimu mkurugenzi wa habari na Mawasiliano na Umma Bw.Ismail Jussa wakati akiongea na waandishi wa habri ikiwa ni siku moja tu baada ya CCM kupitia kikao chake cha halmashuri kuu ya Zanzibar ya CCM kutoa tamko la kuwataka wana CCM kujiandaa na marudio ya uchaguzi ambapo kiongozi huyo wa CUF amesema kauli ya CCM ni ya chama kilichoshindwa na kuwahadaa wananchi huku ikiwahakikishia wanachama na wananchi kuwa CUF italinda matokeo halali ya uchaguzi.
Akizumgumzia mazungumzo yanayoendelea hivi sasa kuhusu mvutano wa mgogoro huo wa kisiasa Zanzibar kaimu mkurugenzi huyo wa habari Ismail Jussa amesema hatua iliyofikiwa ni kubwa  na yako katika hatua za mwisho huku CUF ikiwapongeza wananchi kwa kuonyesha  ukomavu wa kisiasa na kundeleza hali ya amani na utulivu.
CCM na CUF ambavyo ndivyo vyama vikuu vya kisiasa hapa Zanzibar zinaonekana kuzidi kuwachnaganya  wananchi ambao sasa wameingia mwezi wa pili tokea kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi  na zaidi ya  mara sita kwa kamati inayosimamia mggooro huo ambao ina wagombea wawili wa urais wa CCM na CUF na marais wastaafu wa Zanzibar kukutana na hadi sasa hakuna kauli yeyote iliyotolewa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment