Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha
azimio lenye lengo la kukata mifumo ya fedha kwa kundi la Islamic State.
Mkutano wa kwanza wa baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa wa mawaziri wa fedha umeafiki juu ya azimio hilo lililobuniwa kwa ajili
ya kuzuia fedha kuwafikia wanamgambo wa Islamic State.
Mkutano huo umeyataka mataifa kufanya juhudi za
haraka kukata mifumo ya udhamini wa fedha kwa kundi hilo kwa kuzuia wizi wake
wa mafuta na raslimali nyingine.
0 comments:
Post a Comment