Wafanya biashara na wakulima mkoani Morogoro wametakiwa
kufuata vipimo sahihi katika mazao yanayoingia sokoni na kutoka ili kuepuka
utozwaji wa kodi isivyo halali.
Meneja mkoa Wakala Vipimo Morogoro WILSON KACHOLI amesema
kuwa wafanya biashara na wakulima wanatakiwa kutumia vipimo sahihi katika
masoko mbalimbali ili kuepuka utozwaji a kodi kiholela.
KACHOLI amesema kuwa Halmashauri ni uti wa mgongo wa
jamii katika kupambana na ukwepaji vipimo sahihi iwapo watatunga sheria stahiki
kwa watakao kwenda kinyume na agizo hilo.
Meneja huyo ameziomba halimashauri kwa kushirikiana na Ofisi
yake kutenga maeneo maalumu ya kununua na kuuza mazao kwa wakulima na
wafanya biashara ili mchakato wa kufuata vipimo sahihi uweze kuzingatiwa ili
kuepuka unyonywaji kwa wakulima.
Katika hatua nyingine wakulima wamekubaliana na agizo hilo
na kutaka mizani na vipimo vya ujazo kwa wafanya biashara katika massoko
kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara jambo litakalosaidia kuondokana na wizi wa
vipimo hivyo.
Aidhha KACHOLI ametoa wito kwa wafanya biashara katika
masoko yote katika mkoa wa Morogoro kuwasilisha vipimo vyao ili kuepuka
kufungiwa biashara zao.
0 comments:
Post a Comment