Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesema wako tayari
kufikia mapatano ya kuiwezesha Uingereza kusalia katika Muungano huo.
Hata hivyo viongozi hao wanaokutana mjini
Brassels,wamesisitiza kuwa makubaliano yoyote hayapaswi kuvunja kanuni za
muungano wa Ulaya.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema
kumekua na mafanikio,lakini akasema bado kuna kazi ngumu inayowasubiri mbele
yao.
Rais wa Muungano wa Ulaya, Donald Tusk amesema kuwa
viongozi wengine walielezea hofu zao kuhusu mpango wa Uingereza wa kukabiliana
na malipo ya kijamii ya wahamiaji wa Muungano wa Ulaya suala ambalo wengi
wanaliona kama Ubaguzi.
Mkutano huo pia utajadili mzozo wa wahamiaji na
makubaliano kuhusu haja ya kuimarisha mipaka ya nje ya Muungano wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment